Mohammad Hossein Behzadfar na Mohammad Mahdi Rezaei watashindana katika kategoria za kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu na kuhifadhi Juzuu (sehemu) 15.
Hafla hiyo ya kimataifa ya Qur'ani itaanza rasmi katika mji mtakatifu wa Makka Jumamosi, Agosti 10.
Itafanyika katika jumla ya kategoria tano, ikijumuisha viwango tofauti vya kuhifadhi Quran.
Waandalizi walikuwa wametangaza awali kuwa zawadi ni pamoja na kiasi cha SR500,000, SR450,000, na SR400,000 kwa nafasi tatu bora.
Tukio hilo litahitimishwa kwa sherehe katika Msikiti Mkuu wa Makka.
Iran imetuma wawakilishi wake katika hafla ya Qur'ani ya Saudia kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu.
Mwaka jana, mwakilishi wa Saudi Arabia pia alishiriki katika Mashindano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi.
Tehran na Riyadh zilianzisha tena uhusiano wa kidiplomasia mnamo Machi 2023 kupitia makubaliano ya upatanishi wa China, kuashiria maendeleo makubwa baada ya kuvunja uhusiano mnamo 2016.
3489431